Kuzuia na kupunguza viwango vya vifo, majeraha kwa watu, na uharibifu wa mali unaotokana na moto, mafuriko, matetemeko ya ardhi, ajali za barabarani na majanga mengine.
Kutoa Vitambulisho kwa Watanzania na Wageni Wakaazi wa Tanzania na kutunza Daftari la Utambuzi kwa lengo la Kuimarisha Usalama na Amani, Kiuchumi na Kijamii kwa Maendeleo ya Taifa.
Kupokea na kushughulikia malalamiko yanayohusu kazi za Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji, Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Usalama Binafsi.
Kusimamia utekelezaji wa adhabu zisizokuwa za kifungo zinazoendeshwa katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika mikoa yote ya Tanzania Bara chini ya Sheria ya Probation of Offenders (Cap.247 R.E 2002), Sheria ya Huduma kwa Jamii Na.6/2002, na The Extra Mural Penal. Kanuni ya Ajira 1968 (EML) na Sheria ya Bodi za Parole Na. 25/1994.